icono para volver a la página principal Back home

NGUZO KUU Kwa ulinzi wangu, siha njema na ukuaji wangu kama msichana, mvulana au kijana aliyebaleghe anayeishi na ulemavu

1
dibujo del principio 1

NAISHI JINSI NILIVYO NA MIMI NI BINADAMU KAMA WEWE.

Ninapaswa kuheshimiwa na utofauti wangu kudumishwa. Nina haki na hadhi kama yeyote yule.

2
dibujo del principio 2

NAPENDA UKARIMU WAKO, MAPENZI YAKO NA PIA KWA KUWA UNACHEZA NA MIMI

Pia wewe ungependa upendwe na utendewe usawa. Nitakie mema na tufurahie maisha pamoja

3
dibujo del principio 3

NAPENDA UNAVYONITUNZA , KUNILINDA NA KUNIFUNZA JINSI YA KUJILINDA.

Mimi pia nitakujali, kwa njia yangu.

4
dibujo del principio 4

NATAKA UNIKUBALI JINSI NILIVYO, NISAIDIE NIKUZE VIPAWA NA TALANTA YANGU NA UNIPE ELIMU BORA

Nafurahi ukitambua vipawa vyangu na kunisaidia kutangamana na watu wengine.

5
dibujo del principio 5

NAPENDA UNAVYONISIKILIZA, KUNIELEZEA YANAYOTENDEKA PAMOJA NA KUTULIA MAANANI MAONI YANGU.

Hunipa hakikisho na hunisaidia kujifunza na kujiendeleza.

6
dibujo del principio 6

NAPENDA UNAVYONIAMINIA NA KUNIKUZA

Hii inaimarisha imani yangu, uwezo wangu na uhuru wangu.

7
dibujo del principio 7

NAPENDA UNAVYONIELEWA, UNANISAIDIA NA KUNITIA MOYO NIKIWA NIMEUDHIKA, NIKIWA NIMEKASIRIKA AMA NIKIWA NIMESONONEKA

Ni nyakati hizi ndizo ninakuhitaji zaidi.

8
dibujo del principio 8

NAPENDA UNAPONIHUSISHA

Nataka kuishi kwenye mandhari mazuri, yenye utulivu na yanayoutambua ulemavu wangu. Ninegependa pia uniheshimu na uthamini jinsi ninavyowasiliana.

9
dibujo del principio 9

NINGEPENDA UNIHESHIMU NA UNILINDE KUTOKANA NA UKATILI WOWOTE KILA MAHALI NA KWA MANDHARI YOYOTE

Kama yeyote yule, mwili wangu, utu wangu na akili yangu inapaswa kulindwa.

10
dibujo del principio 10

INANIPA TUMAINI UNAVYONIAMINI

Nahitaji kuaminiwa kama wewe.